RIPOTI : SILAHA ILIYOTUMIKA KWENYE KIFO CHA TUPAC YAPOTEA - teknomovies
RIPOTI : SILAHA ILIYOTUMIKA KWENYE KIFO CHA TUPAC YAPOTEA

RIPOTI : SILAHA ILIYOTUMIKA KWENYE KIFO CHA TUPAC YAPOTEA

Share This
Silaha ya moto aina ya A.40 Cliber Glock iliyotumika katika mauaji ya msanii Tupac Shakur ilipatikana miaka 19 iliyopita sasa polisi wanasema hawajui ilipo. Taarifa imetolewa katika ripoti maalum inayoangazia mhusika hawswa wa kifo cha Tupac, "Who Killed Tupac"?
Mwaka 1998 Raia mwema aliokota Bastola hiyo na kuifikisha katika kituo cha polisi ambapo baadae polisi wa Compton waliandikisha kama silaha iliyookotwa mwaka 1998 May 30 .

Kwa mujibu tovuti ya variety.com taarifa  inasema kwamba Mwaka 2000 silaha hiyo ilipelekwa Los Angeles, mwaka 2006 askari polisi T. Brennan alitambua eneo ambalo silaha iliokotwa wakati anachunguza kifo cha Notorious B.I.G akisema kuwa silaha hiyo iliokotwa nje ya nyumba ya mpenzi wa kijana ambae alikuwa kwenye kundi la Crips waliokuwa na beef kubwa na Rapa Tupac.

SOMA PIA : YAFAHAMU MAKUNDI MAHASIMU YA HIP HOP MAREKANI -1

Baada ya  Askari huyo kufanya uchunguzi wa kufananisha risasi zilizotoka kwenye mwili wa 2 pac na zile zile zilizotoka kwenye bastola hiyo akagundua kuwa silaha hiyo ilitumika kumuua Tupac


Mara kwa mara Polisi wamekuwa wakimkwepa kaka yake Tupac ambae amekuwa akifuatilia kwa karibu makala na uchunguzi wa kifo cha ndugu yake huku wakisema silaha hiyo haijulikani ilipo kw sasa.
Karibu kwenye familia ya Teknomovies kupitia Facebook, Instagram na Twitter @ Teknomovies ili uwe wa kwanza kupata mastori makali.

No comments:

Post a Comment

Pages